Mwasiti Aliweka Wazi suala hilo na kusema kuwa wimbo wa 'Nalivua Pendo' ulimuingizia kipato kikubwa kutokana na kukubalika na watu wa Rika lote vijana na Wakubwa ambapo anakiri kuwa hakuwa anatarajia mapokeo hayo wakatiti anauimba.
"Katika nyimbo ambazo zimeniingzia ia pesa nyingi sana katika maisha yangu Nalivua pendo umeniingizia pesa nyingi sana,nilikua nafanya kazi nyingi sana shows nyingi sana ,corporate shows sana kwa sababu ni wimbo wa watu fulani,wakati nautoa mimi nilkua napenda nyimbo za kuruka lakini nkawa najiuliza huu wimbo utafanyaje huu lakini ukawa ni wimbo ambao hata kijana mdogo anaenjoy muziki tofauti na nilivokua nikiuchukulia kua ni wimbo wa watu flani watu wazima na nini " Mwasiti amemuambia Jabir Saleh Mtangazaji wa kipindi hicho.
Wimbo wa Nalivua Pendo ulitoka miaka kadhaa iliyopita na ulikua ni wimbo mkubwa ambao ulimpa mafaniklio msanii huyo toka Kigoma.Kwa sasa Msanii Mwasiti anasikika katika vipindi mbalimbali kupitia wimbo wake mpya alioshirikiana na Rapper Godzilla.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.