0
Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa kiongozi wa kwanza kuondoka katika mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 zenye nguvu kubwa kiuchumi unaoendelea nchini Australia, wakati viongozi wenzake wakijitayarisha kuzindua mpango wao wa kuimarisha uchumi duniani. Putin alikosolewa vikali na viongozi wenzake wa Ulaya kutokana na hatua yake, ya kuingilia mgogoro wa Ukraine. Kati ya waliomkosoa ni pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Kansela wa Ujerumani  Angela Merkel aliyesema huenda Urusi ikawekewa vikwazo zaidi. Suala muhimu katika mkutano huo wa G20 hii leo ni mipango ya kuchochea ukuaji wa uchumi kwa asilimia 2 ifikapo mwaka 2018 hali inayoweza kuongeza nafasi za kazi na kuinua uchumi duniani. Kwa upande mwengine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameyatolea mwito mataifa ya kundi la G20 kushirikiana kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi na kuchangia katika mfuko wa fedha utakaoyawezesha mataifa yanayoendelea kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Post a Comment

 
Top