Merkel awasili Sydney kwa mazungumzo na Waziri Mkuu Tony Abbot
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewasili mjini Sydney
Australia hii leo katika siku ya mwisho ya ziara yake nchini New
Zealand na Australia. Merkel anatarajiwa kuwa na mazungumzo na
Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbot juu ya uhusiano kati ya nchi
hizo mbili. Ziara ya mwisho nchini Australia ilifanywa na Kansela wa
Ujerumani Helmut Kohl mnamo mwaka wa 1997. Katika ziara hii
Kansela Angela Merkel siku ya Jumatatu atakutana na kiongozi wa
Upinzani wa chama cha Labour nchini Australia Bill Shorten kabla ya
kurejea Ujerumani. Australia ni mshirika muhimu wa kimkakati wa
Ujerumani katika kanda ya Asia na Pacific wakati Ujerumani ni
mfanyabiashara muhimu barani Ulaya kwa Australia baada ya
Uingereza.
Post a Comment