Kwa alama hizo, Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano, hivyo kupata shahada ya kwanza daraja la kwanza.
Shahada hiyo inayotolewa katika Shule ya Sayansi ya Asili (CoNaS) chuoni hapo, ni miongoni mwa taaluma adimu nchini. Ilianza kufundishwa chuoni hapo mwaka 2011.
Miongoni mwa taasisi ambazo zitafurahia taaluma hiyo kuanza kupata wataalam nchini ni pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo hulipa fedha nyingi kupata huduma hiyo kwa wataalam kutoka nje ya nchi na kwa gharama kubwa.
Alipopewa nafasi ya kuzungumza mbele ya mamia ya wanafunzi wenzake na wageni waalikwa kwenye ukumbi wa Mlimani City, aliishia kutoa shukrani kwa wahadhiri, wanafunzi wenzake na wote waliomsaidia katika mafanikio yake kitaaluma.
Ili kupata wastani wa ufaulu wa daraja la kwanza kwa kiwango cha GPA ya 4.8, mhitimu hulazimika kufaulu kwa kiwango cha juu kwa miaka yote ya kuwa chuoni. Doreen alifanikiwa kutimiza sharti hilo baada ya kufaulu masomo 32 kwa kiwango cha ‘A’ na masomo mengine sita kufaulu kwa alama za B+ kati ya masomo yote 38 ya shahada yake; baadhi ya yale yaliyomkwamisha kupata A yakiwa ni ‘Actuarial Mathematics’ na ‘Legal Matters in Actuarial Industry’.
Mgawanyo wa ufaulu wake kwa mwaka wa kwanza ulikuwa ni A za masomo 12 na B+ za masomo mawili kati ya masomo 14; mwaka wa pili alifaulu kwa kupata A katika masomo 10 na B+ mbili kati ya masomo 12 na mwaka wa tatu alifaulu pia kwa kiwango cha alama A katika masomo 10 na masomo mengine mawili akapata B+ kati ya masomo 12.
Post a Comment