0
Kipa nambari moja wa Simba, Ivo Mapunda amesema amepanga kustaafu soka akiwa anaichezea timu ya Gor Mahia inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya.
Ivo alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu Desemba mwaka jana, akitokea Gor Mahia baada ya kung’ara katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika nchini humo.
Mapunda alisema amepanga kustaafu kucheza soka miaka michache ijayo akiwa katika timu yake hiyo na kwamba anawasikiliza viongozi wa Simba kama wataamua kutomwongezea mkatabaatarejea Gor Mahia kumalizia soka.

Post a Comment

 
Top