0
Kocha Mkuu wa Coastal Union, Yusufu Chipo, amesema anahitaji kuongeza viungo wa kati wawili katika kikosi chake ili kuimarisha kikosi hicho.
Costal Union kwa sasa inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na jumla ya pointi 11, ikiwa imeshinda mechi tatu, ikipoteza michezo miwili na kutoka sare michezo miwili.
Chipo alisema tayari amewasilisha majina ya wachezaji anaowataka kwa uongozi wake na wachezaji hao wanatoka katika timu za Ligi Kuu na tayari uongozi umeanza mazungumzo na klabu hizo.

Post a Comment

 
Top