Unapozungumzia suala la majeraha ya wachezaji bila shaka mashabiki wa Manchester United wanapata homa ya ghafla .
Hii ni kwa sababu timu hii imekuwa na orodha isiyoisha ya wachezaji wenye majeraha .
Mbaya zaidi ni kwamba kila orodha hii inapoonyesha dalila za kungua mchezaji mwingine anaemia na inazidi kuwa ndefu .
Orodha hii iliongezeka kwenye mchezo dhidi ya Hull City wakati ambapo
kiungo mshambuliaji Angel Di Maria alipoumia misuli ya nyonga kwenye
dakika ya 14 ya mchezo na kulazimika kutoka.
Bado haijafahamika Di Maria atakaa nje ya uwanja kwa muda gani lakini
kwa kawaida jeraha kama hili huhitaji kati ya siku 7 mpaka 10 ili
kupona na wakati mwingine kuendana na ukubwa wake linaweza kuhitaji muda
mrefu zaidi .
Kwa jumla Jeraha la Di Maria ni jeraha la 41 kwa mchezaji wa
Manchester United kwa msimu huu tangu kuanza kazi kwa kocha Mholanzi
Louis Van Gaal .
Idadi hii ndio idadi kubwa ya majeraha kwa wachezaji kwa timu yoyote
ya ligi kuu ya England msimu huu hali inayowafanya United waamini kuwa
huenda timu yao ina mkosi wa aina Fulani.
Post a Comment