
Mchezaji wa zamani wa timu ya Brazil Pele
anendelea kupata afueni lakini bado amelazwa katika chumba cha wagonjwa
mahututi akiwa na maambukizi ya eneo la kupitisha mkojo mapema wiki
hii.Habari hizo zinajiri baada ya gwiji huyo wa soka kusema katika
mtandao wa twitter kwamba anaendelea kupata afueni katika hospitali moja
ya Albert Einstein iliopo mjini Sao Paulo.Hatahivyo msaidizi wa mzee
huyo mwenye umri wa miaka 74, Jose Fornos alipuuzia habari hizo.Lakini
hospitali hiyo imesema kuwa Pele anaendelea kupata msaada wa muda wa
figo yake na kwamba hahitaji usaidizi wowote wa kupumua.Taarifa hiyo
iliongezea kwamba mchezaji huyo wa zamani anaendelea kupata afueni na
kwamba bado amesalia katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Awali Hospitali hiyo ilikuwa imesema kwamba Pele alikuwa amelazwa na akiwa hali mbaya.
Lakini baadaye Pele akaandika kwamba
yu buheri wa afya katika mtandao wake wa Twitter na alikuwa amehamishwa
hadi chumba maalum ndani ya hopsitali hiyo kutokana na maswala ya
faragha.
Aliongezea kwamba ijapokuwa
anawashukuru wale wote waliomtembelea kumpa pole ,alitaka kuendelea na
matibabu yake kwa njia ya amani.
Amesema kwamba angependa kuwa na
familia yake wakati wa sikukuu na ataanza mwaka mpya akiwa katika afya
nzuri huku ziara nyingi za kimataifa zikiwa tayari zimepangwa.
Post a Comment