Kiungo mbrazil Emerson De Oliviera Neves Roque (kushoto) akisaini
mkataba leo wa kuitumikia klabu ya Young Africans, kulia ni Afisa Habari
wa klabu Baraka Kizuguto.Kiungo Emerson De Oliveira Neves Roque leo
amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Young Africans baada
ya benchi la ufundi kuridhika na uwezo wake,na mchezaji mwenyewe
kufikia makubaliano hayo ya kuwatumikia watoto wa Jangwani.Baada ya
kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo chini ya makocha Marcio Maximo,
Leonardo Neiva na makocha wazawa Salavatory Edward, Shadrack Nsajigwa
kwa pamoja wameridhiswa na uwezo wake na kuomba apewe kandarasi la
kuitumikia klabu ya Young Africans.
Emerson aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja
la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji
Geilson Santos "Jaja" ambaye ameshindwa kureje nchini kutokana na
matatizo ya kifamilia na kuomba klabu ya Young Africans imuache.
Kocha wa Young Africans Marcio Maximo amesema wamerizishwa na uwezo
na kiungo mkabaji Emerson na kusema ataisaidia timu katika michuano
mbali mbali ya Ligi na Kimataifa.
Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Young Africans kufikisha jumla ya
wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna
Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.
Post a Comment