Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki, Meneja
Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza (pichani), alisema kumejengeka
utamaduni kwa wananchi hasa katika maeneo ya mijini kutumia mifuko hiyo
kuhifadhi vyakula vya moto kama chips na wali bila kujali madhara yake.
“Mifuko ya plastiki imetengenezwa kwa kemikali ambazo zinaweza
kumletea madhara mlaji kutokana mwingiliano kati ya chakula na kemikali
hizo, ni vyema wananchi wakaelewa kinga ni bora kuliko tiba,” alisema
Simwanza.
Aidha, aliwataka wananchi na wauzaji wa vyakula kuelewa kuwa, kuna
mifuko maalum iliyotengenezwa kwa ajili ya kuwekea na kubeba vyakula vya
moto, huku akiwasisitiza mifuko hiyo inafaa kuhifadhi vyakula visivyo
vya moto.
Alisema wauzaji wa vyakula wanatakiwa kutumia vifaa
vilivyotengenezwa kuhifadhi na kubebea vyakula ili kuwalinda wateja wao
wasipatwe na magonjwa yanayoweza kusababishwa na mifuko hiyo.
Post a Comment