0
Rais al Bashir awajibu wanaotaka kususia uchaguziRais wa Sudan amesema kuwa mwito wa wapinzani wa nchi hiyo wa kususia chaguzi za rais na bunge hauna umuhimu.
Rais Omar al Bashir wa Sudan amesema katika radiamali yake kufuatia hatua ya vyama vya upinzani nchini humo ya kuwatolea wito wananchi kususia chaguzi za rais na bunge kwamba, vyama vya upinzani nchini Sudan haviwezi kushindana na chama tawala kupitia masanduku ya kura na ndio maana vinataka kususia chaguzi hizo.
Katika upande mwingine Rais al Bashir amesema kuwa, awamu kuu ya mazungumzo ya kitaifa ya Sudan itaanza hivi karibuni na kwamba mazungumzo hayo yatahudhuriwa na waangalizi kutoka taasisi za kimataifa.
Muungano unaoundwa na vyama vinavyoipinga serikali ya Sudan na harakati za waasi wanaobeba silaha, umetaka kususiwa chaguzi za rais na bunge zilizopangwa kufanyika nchini Sudan tarehe 13 Aprili mwaka huu.

Post a Comment

 
Top