Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein
amesema ili mahakama zifanye kazi zake kwa uadilifu na ziendelee kuwa
huru mihimili mengine haipaswi kuingilia katika maamuzi yake inayotoa
na kutaka itekezwe.
Dkt
Shein ametoa kauli hiyo hapa Zanzibar wakati akihutubia katika siku ya
sheria Zanzibar ambayo ilifanyika katika viwanja vya bustani ya
Victoria na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria
wakiwemo majaji, mahakimu, wanasheria na mawakili wakiongozwa na makamu
wa pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi pamoja na Jaji mkuu wa Tanzania
Omar Chande.
Dkt Shein aliwataka majaji na mahakimu kufanya kazi yao bila ya hofu na bila ya upendeleo huku akiwataka wananchi kufanya juhudi za kuzielewa na kuzifuata sheria.
Mapema katika siku hiyo ya sheria Zanzibar wakuu wa sekta hiyo muhimu za sheria walipata fursa ya kutoa salamu zao ambapo mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan alisisitiza umuhimu wa Katiba na utawala bora huku Rais wa chama cha wanasheria Zanzibar Awadh Ali Said alishauri serikali kuanzisha mfuko maalum wa utendaji wa mahakama.
Naye Jaji mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Makungu kwa upande wake amesema bado tatizo la rushwa limekuwa ni sugu ingawa mahakama imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana nayo.
Sherehe hizo za siku ya sheria Zanzibar ambazo mwaka huu kauli mbiu ni mahakama huru, msingi na utawala bora

Post a Comment