Sehemu
ya barabara ya Ndundu –Somanga(KM 60) iliyokamilika kwa kiwango cha lami
Wanahabari
wakimhoji Dereva wa basi la abiria kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam
kuhusiana na kukamilika kwa sehemu ya barabara hiyo.
Habari na picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi
Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kukamilika kwa barabara ya
Ndundu- Somanga (Km 60) na kuwataka wakazi wa mikoa ya kusini kuitumia
vizuri barabara hiyo kuibua fursa za kiuchumi na hivyo kujiletea
maendeleo.
Dkt.
Magufuli alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam mara baada ya
kukamilika kwa ukaguzi wa barabara hiyo uliofanywa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe.
“ Wito
wangu kwenu wakazi wa mikoa ya kusini ni kuitunza barabara hii ili idumu
kwa muda mrefu na kuibua fursa za kiuchumi zitakazo wawezesha kupata
maendeleo na kupunguza umaskini” alisisitiza Waziri Magufuli.
Kufatia
kukamilika kwa barabara hiyo, Dkt. Magufuli ameishukuru Wizara ya Ujenzi
pamoja na Wakala wa Barabara Nchini, (TANROADS), kwa kazi kubwa ya
kusimamia kazi hiyo iliyodumu kwa muda mrefu kutokana na changamoto
mbalimbali.
“Nampongeza
Katibu Mkuu wa Wizara pamoja na Mtendaji Mkuu wa TANROADS kwa usimamizi
makini uliosababisha kukamilika kwa mradi huu muhimu utakaoleta
ukombozi kwa wakazi wa mikoa ya kusini” alisema Waziri Dkt.Magufuli
Kwa
upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe ameelezea
kuridhishwa kwake na ujenzi wa barabara hiyo na kuwaomba wananchi
kuitunza ili idumu kwa muda mrefu.
“Barabara hii imekamilika kwa kuchelewa lakini imezingatia viwango
vilivyowekwa kimkataba hivyo nawasihi madereva na wananchi kuitumia kwa
uangalifu ili kuepuka ajali na kuibua fursa za maendeleo” alifafanua
Eng. Iyombe
Barabara
ya Ndundu-Somanga ni sehemu ya barabara kuu ya Dar-Es-salaam
-Lindi-Mtwara ambayo imekuwa kwenye matengenezo kwa muda mrefu na Ujenzi
wake umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 60.
Post a Comment