Wakulima
wa mpunga Mkoani Mbeya wameshauriwa kukata Bima ya Mashamba yao ili
kuepuka hasara wanayoweza kuipata punde mazao yao napoharibika kwa
ukame, viwavijeshi au majanga mengine yatokanayo na mabadiliko ya hali
ya hewa.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda alipotembela Mashamba ya mpunga Mkoani Mbeya
Akitoa
elimu juu ya kilimo cha mkataba, kwa ajili ya wakulima wa mpunga wa
kata ya Chitete wilayani Momba kupewa mbegu na pembejeo za kilimo ili
waweze kuzalisha mazao bora yanayokidhi mahitaji ya soko, mkurugenzi wa
kampuni ya mtenda kyela rice, George Mtenda amewashauri wakulima hao
kuhakikisha wanakata bima ya mashamba yao ili inapotokea wakashindwa
kuvuna kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa
waweze kufidiwa gharama zao.
Afisa ughani wa kata ya Chitete, Samson Mwasote amesema kuwa wakulima wengi wa kata hiyo wamekuwa wakilima bila kutumia mbolea wala ushauri wa kitaalam kutokana na kukosa uwezo wa kiuchumi wa kupata pembejeo, hivyo wakisaidiwa kwa kupewa mbegu bora na pembejeo wataongeza uzalishaji mara dufu
Baadhi ya wakulima wamesema kuwa utaratibu wa kukata bima ya mashamba yao ni mzuri na utawasaidia kulima kwa kujiamini na bila woga wa kuzikimbia familia zao punde wanapopata hasara wakiogopa kulipa madeni ya pembejeo walizokopeshwa.

Post a Comment