LOUIS
van Gaal amekumbwa na majanga ya majeruhi licha ya Manchester United
kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi yaYeovil Town katika mechi ya
raundi ya tatu ya kombe la FA.
Rafael
da Silva alivujika mfupa wa taya katika kipindi cha kwanza na kutolewa
wakati wa mapumziko, wakati mlinzi mwenzake Paddy McNair alihitaji
bandeji kichwani kufuatia kugongana na Kieffer Moore.
Van
Gaal pia alieleza kuwa beki mwingine Luke Shaw alipata majeraha mapya
ya kifundo cha mguu na yeye alitolewa wakati wa mapumziko baada ya
kucheza kwa kutumia dawa ya kuzuia maumivu.
Post a Comment