Kiungo
raia wa Cameroon anayekipiga kwa mkopo kwenye klabu ya West Ham United
akitokea klabu ya Barcelona ya nchini Hispania Alex Song ametangaza
kupitia mtandao wake wa tweeter kuwa ameamua kujiuzuru kuitumikia timu
yake ya taifa.
Song ameonekana kutoridhishwa na kitendo cha mara kadhaa kutemwa kwenye kikosi cha timu hiyo ya taifa na hivyo kuamua kujiweka pembeni ili awapishe wachezaji chipukizi waoneshe uwezo wao.
"
Tangu kumalizika kwa michuano ya kombe la Dunia kule nchini Brazil
kumekuwa na hali ya mimi kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa mara
kadhaa, Lakini kubwa zaidi ni hili la mimi kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kwaajili ya michuano mikubwa kabisa ya Afrika inayotarajiwa kushika kasi mwaka huu."
"Kumekuwa
na mazungumzo baina ya chama cha soka ma meneja wa timu ya taifa ili
niweze kujumuishwa kwenye kikosi hicho lakini mimi binafsi nimeonelea ni
bora nikae pembeni kulikoni kulazimisha jambo ambalo meneja wa timu ya
taifa linalotazamwa na watu wengi zaidi halitaki."
"Nafahamu
kuwa ni mapema sana kwa mchezaji wa umri wangu kutangaza najiuzuru
kuitumikia timu yangu ya taifa na mimi binafsi najisikia vibaya sana kwa
jinsi hali ya mambo yanavyokwenda lakini nitafanya nini na mazingira
ndio yako hivyo ambavyo tumeyaona
Post a Comment