0
Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na Serikali ya Tanzania kupitia mpango wa Rais Jakaya Kikwete wa kusaidia maeneo yenye uhitaji maalum wa ufunguaji wa fursa za kiuchumi kwa jamii za pembezoni, umeanza utekelezaji wa mradi wa  kuijenga upya miundo mbinu ya barabara za vijiji 11 vya jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro.

Miundombinu na Jiografia ya barabara zilizopo kwenye jimbo hilo, lililopo kwenye safu ya juu ya milima ya Upare, ilikuwa ikiwakosesha wakazi wa milimani fursa ya kufurahia mawasialino hayo na wakazi wengine wa maeneo ya tambarare kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali ikiwamo ikiwamo kufuata huduma za rufaa kwenye hospitali ya wilaya hiyo, umbali wa zaidi ya kilomita 93.

Mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango Malecela (CCM), akitoa taarifa ya hatua ya ujenzi huo ulikofikia kwa sasa, alisema uamuzi wa Rais Kikwete kujenga barabara mpya na kuzihuisha za zamani kwa kuitanua miundo mbinu katika maeneo korofi na yenye jiografia utayafanya maeneo hayo kuwa eneo salama la kuishi kwa zaidi ya miongo.

Alizitaja barabara zilizopo kwenye mradi huo maalum wa Rais Kikwete ni Miyamba, Mshiwi –Kambene-Ndolo na Paraine-Kitibwa,Kirongwe na Mpinji pamoja na barabara ya Kiwandani-Manga, Chalinze ambazo ujenzi wake unagharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili.

“Wanaosema kwamba Rais Jakaya Kikwete na serikali yake hawajafanya kitu ni wanastahili toba; bila ya huruma yake maeneo haya yasingefunguka huko tuendako…Mungu amzidishie afya njema kwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa Oktoba 29 mwaka 2012 alipowatembelea waathirika wa maporomoko,” alisisitiza Kilango.

Post a Comment

 
Top