TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 20.11.2014.
- WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI PAMOJA NA MICHE YA BHANGI.JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA NYAKATI TOFAUTI WAKIWA NA BHANGI PAMOJA NA MICHE YA BHANGI. KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KATSON IYISEGA (68) MKAZI WA KIJIJI CHA ISWAGO ALIKAMATWA AKIWA AMEOTESHA MICHE YA BHANGI 12 KATIKA SHAMBA LAKE LA MAHINDI. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.11.2014 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISWAGO, KATA YA SANTILYA, TARAFA YA ISANGATI, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BHANGI NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
AIDHA KATIKA MSAKO WA PILI,
MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BRYSON
SANGA (28) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI
KETE 15 SAWA NA UZITO WA GRAM 75.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.11.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO
KATIKA ENEO LA NSALAGA – UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI
NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI, TARATIBU
ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA
ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA
ULIMAJI WA BHANGI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI
YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment