
Isitoshe, Nyalandu aliongelea utawala wa Rais Kikwete kuwa ni utawala
unaolindwa na majini saba, ingawa hakufafanua alimaanisha nini, lakini
alishangiliwa sana na waumini wa Efata.
Anayejiita nabii na mtume Mwingira, naye aliongeza kuonesha wazi kuwa
Nyalandu ndie chaguo lao.My take: Huo ni udini wa wazi kabisa. Nyalandu
ameanza kutumia kanisa analosali kuomba kura za waumini wake.Kuna
maneno ambayo yamemkosea adabu Mwenyekiti wa CCM, Professa Kikwete,
kwamba analindwa na majini saba. Sina hakika kama maneno hayo ni rasmi
ndani ya CCM au ni ya kanisa la Mwingira.
Wadau karibuni.
Source: Star TV live broadcast Mkesha wa mwaka mpya.
Post a Comment