Baadhi ya wananchi mkoani Kagera
wamepinga uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk
Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani waziri wa ardhi nyumba na
makazi na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiri kuhujumu pesa za
akaunti ya
Tegeta Escrow.
Wakiongea na mwandishi mwetu,
wananchi wa mkoa huo wamesema hawajajua nini hatima ya Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania Dk. kikwete kwa kuwaweka Kiporo mawaziri wengine
waliohusika katika sakata hilo na kumuuondoa waziri
Tibaijuka na pia wamebaki na sintofahamu ambapo wamemtaka
Rais kutoa ufafanuzi kuwa licha ya kumng’oa madarakani kiongozi
huyo Je, Pesa hizo zitarudishwa kwenye akaunti hiyo ya Tegeta
Escrow au la.
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya
siasa vya mkoa huo akiwemo katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha
Mapinduzi mkoa wa Kagera Hamimu Mahamudu amepongeza uamuzi wa Rais
alioutoa wakati akiongea na wazee wa jijini Dar es salaam kwa
kumuondoa kiongozi huyo.
Kwa upande wake, katibu wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika manispaa ya Bukoba Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahii ambapo amemtaka Rais kuwafahamisha watanzinia kuwa Pesa za Escrow zitarudishwa lini katika akaunti hiyo au kuwaondoa viongozi hao madarakani ndio suluhisho na kwamba pesa hizo hazirudishi?.

Kwa upande wake aliyekuwa
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka amesema
licha ya Rais kumuondoa katika nafasi yake aliyokuwa nayo sasa
amerudi jimboni kwake kwaajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali
za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi ya
kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na kwamba Pesa hizo alizopewa na
Rugemalila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama
pesa hizo zilitoka katika akaunti ya Tegeta Escrow ndo maana hakutaka
kujiuzulu.
Post a Comment