Boti ya polisi
iliyokuwa katika doria mashariki ya mkoa wa kusini Unguja eneo la Jambiani
imegonga, mwamba na kusababisha askari waliokuwemo kutoswa baharini huku mmoja
akifariki
na mwengine hajaonekana.
Akizungumza na
waandishi wa habari kamishna mkuu wa jeshi la polisi CP Hamdan Omar Makame
amesema boti hiyo inayoitwa ushirikiano ilikuwa katika doria ya kawaida na
ndipo ilipokutana na dhoruba hiyo na ilikuwa na askari sita ambao mmoja wao
akiwa ni afisa wa KMKM na wanne waliweza kuokolewa nammoja kufariki ambaye ni
Said Hassan Saleh na hadi sasa kikosi cha polisi cha baharini kianendelea
kumtafuta afisa wa Polisi Asp Tenga Seleamn Pandu bado hajaonekana na juhudi
zinaendelea kumtafuta.
Akizungumzia silaha zilizokuwandani ya boti hiyo ambayo ni miongoni mwa boti zilizotolewa msaada na serikali ya Marekani CP Hamdan Omar Makame amesema silaha zote zimepatikana naziko salama na hali ya boti hiyo iko salama na inatarajiwa kuletwa makao makuu ya kitengo cha baharini ili ichunguzwe.
Wakati mwaka 2014 unakaribia kumalizika ajali hiyo ya baharini iliyoikumba boti ya doria ya polisi inaingia katika miongoni mwa ajali zilizosababisha vifo katika mwaka 2014 hapa Zanzibar.
Post a Comment