0


Mnangagwa, Mugabe na Mujuru
Mnangagwa, Mugabe na Mujuru
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemteua Waziri wa Sheria wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa, kuwa mrithi wake.
Emmerson Mnangagwa, ameteuliwa Jumatano Desemba 10 mwaka 2014 kuwa naibu mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU-PF, na makamu wa rais wa taifa la Zimbabwe. Nafasi hiyo ni mhimu, wakati ambapo rais Mugabe ana umri wa miaka 90.

Iwapo kifo kitamkuta Robert Mugabe hakuna shaka, mrithi wake ndiye atapaswa kuchukua madaraka ya uongozi wa nchi.

Emmerson Mnangagwa, ni mshirika wa karibu wa Robert Mugabe. Aliwahi kuhudumu kwenye wizara muhimu. Aliwahi kuwa Waziri wa Usalama wa taifa, Waziri wa ulinzi na Waziri wa sheria.

Emmerson Mnangagwa ni mtu anayeogopwa. Aliwahi kukomesha machafuko ya watu waliokua walijitenga katika majimbo ya Matabeleland na Midlands baada ya uhuru. machafuko hayo yalisababisha vifo vya watu 20, 000. Mnangagwa alijua baadaye kuwa alifundishwa " kuharibu na kuua" kabla.

Huenda akawa mmoja kati ya watu tajiri katika utawala wa Mugabe, akipata faida hususan katika migodi ya dhahabu.

Kulingana na mwanadiplomasia mmoja wa Marekani, kiongozi huyo alipata utajiri, kufuatia dhahabu alizo kua akijizolea wakati alipomsaidia rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Laurent Kabila, kupambana na waasi nchini humo.

Miezi ya hivi karibuni, Mnangagwa, alishirikiana na mke wa Robert Mugabe, Grace Mugabe, ili wamuangushe Joice Mujuru kwenye wadhifa wa Waziri mkuu tangu miaka kumi iliyopita.

Rais wa Mugabe alimfuta kazi Makamu wake Joice Mujuru kwa madai ya kupanga mbinu za kumuua na pia kuhusika na kashfa za ufisadi.

Pamoja na Bi Mujuru, rais Mugabe aliwafuta kazi Mawaziri 7 waliokuwa wanaegemea upande Makamu wa rais.

Bi Mujuru alikanusha madai kuwa alikuwa anapanga njama za kumuua rais Mugabe kama ilivyodaiwa na mke wa rais Grace.

Mbali na kufutwa kazi kama Makamu wa rais, Bi Mujuru ambaye wakati mmoja alioneakna kuwa huenda akawa mrithi wa Mugabe, pia aliondolewa katika Kamati Kuu ya chama cha ZANU-PF.

Miongoni mwa Mawaziri ambao walifutwa kazi ni pamoja na Waziri wa Usalama wa ndani, Didymus Mutasa, ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Mugabe na Waziri wa Nishati, Dzikamai Mavhaire, mshirika wa karibu wa Bi Mujuru.

Kwa muda wa miezi mitatu sasa rais Mugabe na Makamu wake wa rais, hawajawa na uhusiano mzuri, na kuondolewa kwake katika wadhifa huo hakujawashangaza wananchi wa Zimbabwe.

Post a Comment

 
Top