Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Farasser Kashai, alisema wahamiaji hao ambao hawajui lugha ya Kiingereza wala Kiswahili walikamatwa juzi katika kijiji cha Kicheba wilayani Muheza.
Kashai alisema kuwa wahamiaji hao walikamatwa na askari mgambo baada ya kupata taarifa kutoka kwa watu wema.
Alisema wahamiaji hao walikuwa wamehifadhiwa katika nyumba ya kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mkongo ambaye ametoroka na familia yake baada ya tukio hilo.
Kashai alisema kuwa watu hao bado hawajatambuliwa majina yao kutokana na kushindwa kuwasiliana kwa lugha ya Kiswahili wala Kiingereza.
Alisema wanafanya mpango wa kupata mkalimani ili kuwahoji. Kashai alisema kuwa baada ya Wahabeshi hao kukamatwa wilayani Muheza wamepelekwa Tanga mjini kwa mahojiano zaidi.
Alisema kuwa anawaomba wananchi kutoa taarifa kwa wahamiaji hao haramu ambao wanahifadhiwa na watu na kutoa onyo mtu atakayekamatwa amewahifadhi atachukuliwa hatua.
Wilaya ya Muheza imekuwa ikikamata wahamiaji haramu ambao wanahifadhiwa na wenyeji wa hapo ambapo madereva wa bodaboda wamekuwa wakiwasafirisha.
Post a Comment