0

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, mkoani Kilianjaro  imelazimika kuhairisha kesi  ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Erasto Msuya (43) aliyeuawa kwa kupigwa risasi 13 Julai mwaka jana.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kutajwa jana, lakini ilishindikana  kutokana jaji aliyetarajiwa kuisikiliza kupata tatizo la afya ghafla na kulazimika kwenda kupumzika Akizungumza na NIPASHE, msajili wa Mahakama hiyo, Huseni Mushi , alisema jaji Benedick Mwingwa, alishindwa kuendesha kikao cha mahakamakutokana na sukari na presha kupanda  ghafla akiwa anajiandaa kuingia katika chuma cha mahakama.

”Jaji amepatwa na tatizo la kiafya na kulazimika kuhairisha kesi zote zilitotarajia kusikilizwa leo kwa lengo la kumpa nafasi ya kutosha kupunzika,” alisema Mushi.
Wafanyabiashara wadogo wa madini, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Erasto Msuya a.k bilionea Msuya, walifurika  mahakamani.

Makachero wa polisi  walikuwa wameimarisha usalama  katika kila kona ya mahakama hiyo na kufanya ukaguzi kuhakikisha  hakuna mwananchi yeyote anayeweza kupenya na silaha.

Mushi alisema kesi hiyo imehairishwa mpaka Mahakama itakapojadili na kupanga tarehe nyingine.

Post a Comment

 
Top