
Mawaziri waliotajwa kwenye kashfa hiyo ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao ni miongoni mwa viongozi waliotajwa katika kashfa hiyo na kupendekezwa na Bunge Novemba 28, mwaka huu wavuliwe nyadhifa zao.
Viongozi waliotajwa katika kashfa hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala ya Bunge, William Ngeleja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, Andrew Chenge.
Ingawa haikuelezwa sababu za mabadiliko hayo, hivi karibuni kumetokea mapigano ya wakulima na wafugaji mkoani Manyara na wilayani Kisarawe Pwani baina ya wafugaji kwa Kimang'ati na Wasukuma na kusababisha baadhi yao kuuawa na wengine kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa jana Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi Ombeni Sefue, Rais Kikwete amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Daudi Felix Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wakuu wa mikoa waliohamishwa na vituo walivyofangiwa kwenye mabano kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo (Simiyu).
Mbwilo anachukua nafasi ya Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Nkaya Bendera (Manyara) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk. Rajabu Rutengwe (Morogoro).
Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Magalula Saidi Magalula (Tanga), Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Bakari Mahiza (Lindi) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhandisi Evarist B. Ndiliko (Pwani).
Mabadiliko hayo yamefanyika takribabi mwezi mmoja tu tangu Kikwete alipofanya mabadiliko mengine ya wakuu wa mikoa, Novemba 5, mwaka huu.
Post a Comment