Baada ya kukamilisha zaira hiyo bwana Nabarro amesema ameridhishwa na kiwango cha makabiliano dhidi ya Ebola lakini akatoa angalizo.
“Yafuatayo ni lazima kabisa. Lazima tuelimishe, tuwe macho na
kuendeleza juhudi hadi ifike hatua kila mwenye maambukizi ya Ebola aweze
kutibiwa na kisha kirusi kitoweke. Kwa hiyo kuwa macho ni muhimu sana
vinginevyo mambo yatakuwa mabaya zaidi kama ilivyokuwa mwezi Agosti na
Septemba.”Mjumbe huyo maalum anaelekea nchini Mali moja ya nchi zilizothibitishwa kuwa na visa vya homa kali ay Ebola.
Post a Comment