
Chanongo aliyemaliza sakata lake na uongozi wa klabu hiyo la utovu wa nidhamu sasa atalazimika kujifua zaidi ili amridhishe kocha Phiri ambaye anapambana kuirejesha Simba katika kiwango bora na matokeo ya kuridhisha baada ya kuanza msimu wa ligi kuu 2014/15 kwa matokeo ya sare mfululizo sita kabla ya kupata ushindi katika mchezo wa raundi ya saba.
Msemaji wa Simba Hamphrey Nyasio amesema kiwango cha Chanongo kwasasa hakipo katika hali nzuri na kwamba amepewa muda wa kurekebisha kiwango hicho kupitia kikosi cha pili na kwamba jitihada zake ndizo zitakazo mrejesha katika kikosi cha kwanza.
“Mwalimu ameamua kumpeleka Chanongo kikosi cha pili, kwakuwa kiwango chake kimeshuka hivyo jitihada zake ndizo zitakazo mshawishi kocha Phiri kumrejesha kikosi cha kwanza”
Aidha Nyasio amesema kikosi cha Simba kinaendelea vema na mazoezi yake kabla ya mchezo wa mtani Jembe dhidi ya Yanga mwezi ujao, na kwamba wachezaji wote wako katika hali nzuri mbali na Hussein Sharifu ‘Casillas’ambaye bado anafanya mazoezi mepesi.
Post a Comment