Chama
cha mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam BD, kimesema kimejiandaa
kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazojitokeza katika mzunguko wa
pili wa Ligi ya Kikapu mkoa wa Dar es salaam RBA inayotarajiwa kuanza
kutimua vumbi Junuari 6 mwakani
Akizungumza
na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa BD, Richard Julles amesema
wamefanya mabadiliko makubwa kwa ajili ya kuhakikisha wanapambana na
changamoto zilizokuwa zikitatiza ligi katika mzunguko wa Kwanza.
Julles amesema vilabu pia vinajua changamoto zilizokuwepo pamoja na ugumu wa ligi hivyo itawasaidia kuweza kupambana na kuboresha ili kuweza kuiboresha zaidi.
Julles amesema vilabu pia vinajua changamoto zilizokuwepo pamoja na ugumu wa ligi hivyo itawasaidia kuweza kupambana na kuboresha ili kuweza kuiboresha zaidi.
Post a Comment