Baada
ya kuachia 'Siri' kazi kali kabisa ya pamoja kutoka kwa Barnaba Classic
pamoja na Vanessa Mdee, mastaa hawa wamesema kuwa, mchakato wa video ya
kazi hii umepangwa kufanyika huko Afrika Kusini hivi karibuni.

wasanii wa miondoko ya bongofleva Vanessa Mdee na Barnaba
Ikiwa
ni moja ya kazi ambayo imepata kuzungumzwa sana mtandaoni kutokana na
ubora na utata wa kava lake, Barnaba ameahidi video ya aina yake kwa
wapenzi wa muziki.
Kwa upande wa Vanessa, staa huyu amesema imekuwa ni uzoefu wa aina yake kufanya kazi na Barnaba ambaye amekuwa pia msaada mkubwa katika kumrekebisha hapa na pale ili kukamilisha kazi hiyo katika kiwango kinachotakiwa.

Post a Comment