Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Said Meck Sadiki Meli kubwa ya mizigo iliyobeba Kivuko kipya cha
MV Dar es Salaam ilipokuwa inakaribia kutia nanga katika bandari ya Dar
es Salaam.
Taaswira
ya Kivuko cha MV Dar es Salaam kama kinavyoonekana juu ya Meli kabla ya
kushushwa majini katika bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionesha furaha yake ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki kulia akiwa pamoja na Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa
Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA Eng. Japhet Masele
kuhusu vitu mbalimbali ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.
Waziri wa
Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Marcellin Magesa kwa kazi nzuri
ya upatikanaji wa Kivuko hicho kipya na cha kisasa cha MV Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwa ndani ya chumba cha Nahodha wa Kivuko hicho.
Mhandisi Masele akitoa maelezo kuhusu kamera maalumu kwenye Kivuko hicho.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua boya la kujiokolea ndani ya siti mojawapo ndani ya Kivuko hicho kipya.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki wakwanza kushoto akiwa na Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Marcellin
Magesa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe
wakiteta jambo kabla ya kuwasili kwa kivuko hicho kipya .
Waziri wa
Ujenzi akishuka kwenye ngazi mara baada ya ukaguzi huo.Picha zote kwa
Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU) Wizara ya Ujenzi.
Post a Comment