Kijana Nicholas Mhagama (25) aliyejilipuwa na mafuta ya taa akidai kunyanyaswa.AJILIPUA KWA MAFUTA YA TAA
Kijana
mmoja Nicholas Mhagama (25), mkazi wa Makongo Juu Dar, juzi kati
alijilipua na mafuta ya taa kisa kikidaiwa kunyanyaswa na babu yake.
Tukio hilo lilitokea eneo la Makongo Juu Makaburini usiku ambapo kijana
huyo na babu yake aliyemtaja kwa jina moja la Mhagama waligombana.Baada
ya kijana huyo kuona isiwe tabu alijilipua na mafuta ya taa alipoona
maumivu yanazidi akaanza kupiga kelele za kuomba msaada ambapo
aliokolewa na kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala na baadaye kuhamishiwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuwa mbaya.
Waandishi walikwenda kufanya mahojiano naye hospitalini hapo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ndugu zangu naomba mnisaidie nipone kwani uamuzi niliouchukua haukuwa sahihi ni hasira za kilevi nilichokuwa nimekunywa.
“Yote
haya ni sababu ya manyanyaso niliyopata kutoka kwa babu yangu ambaye
alinifukuza nyumbani na kunitaka nikapange nyumba wakati nilikuwa na
matatizo ambayo alikuwa akiyajua,” alisema Mhagama.
Post a Comment