Jengo moja la gorofa laporomoka huko Zanzibar katika eneo la kihistoria Jaws Corner ndani ya manispaa ya mji mkongwe Zanzibar.
Taarifa
zinasema wananchi wa karibu na eneo hilo wakishirikiana na vikosi
maalumu vya serikali vinaendelea kufanya jitihada mbali mbali katika
eneo hilo ikiwemo kuhakikisha hakuna athari zaidi zitakazoweza kutokea.
Baadhi
ya shuhuda mmoja ameiambia mazrui media kuwa watu wana wasiwasi juu ya
uwepo wa watu wawili waliokua wakipita njia hawana uhakika kama waliwahi
kuvuka au laa.
Hadi
sasa juhudi za kuondoa kifusi cha jengo hilo kimeanza ili kuweza
kubaini kama kuna watu wowote wale waliojeruhiwa au kupoteza maisha.

Post a Comment