Jeshi la Nigeria limeukomboa mji wa Chibok huko kaskazini
mashariki mwa nchi hiyo kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram.
====.
Viongozi wa kundi la G20 la nchi zenye nguvu kubwa za
kiuchumi duniani leo wamejitolea kuzifanyia mageuzi, hatua za kukuza uchumi kwa
pamoja kwa asilimia 2.1 kufikia mwaka 2018 licha ya kuwepo kwa ushahidi wa
kushuka kwa uchumi katika baadhi ya mataifa makubwa.
===.
Afisa mmoa wa Ujerumani amesema mwanadiplomasia wa nchi hiyo
anayefanya kazi mjini Moscow amefukuzwa muda mfupi baada ya mwanadiplomasia wa
Urusi anayefanya kazi mjini Bonn kufukuzwa kutokana na ripoti za vyombo vya
habari kwamba ni mpelelezi.
=====.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Mbowe, amesema hana ugomvi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe,
kwa kuwa amemlea na amemesaidia vitu vingi zikiwamo fedha, gari, kula na kulala
nyumbani kwake.
===.
Mgogoro mkubwa wa kugombea malisho umeibuka katika kijiji
cha Miti Mirefu, wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, baina ya jamii ya kifugaji
ya Kimasai na Mwekezaji katika shamba la Ndarakwai, na kusababisha ugomvi hata
kuzua hali ya wasiwasi katika eneo hilo ambapo magari tisa yameteketezwa kwa
moto huku nyumba zaidi ya 16 zikichomwa moto.
=======.
Nahodha wa England, Wayne Rooney alifunga bao la mkwaju wa
penalti na kumfanya kushika nafasi ya 3 katika listi ya wafungaji bora wa muda
wote wa ‘ The three lions’. England ilishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Slovenia,
jana Jumamosi katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za ulaya, 2016,
Ufaransa.
======.
Manchester United walikuwa tayari kumfanya Gareth Bale
mchezaji ghali zaidi duniani lakini winga huyo alipiga chini wazo hilo na
kuamua kutimiza ndoto yake ya kujiunga na Real Madrid, wakala wake Jonathan
Barnett amethibitisha.
=========.
Post a Comment