Makadirio hayo yanatokana na mtindo mpya ulioundwa na watafiti wa vyuo vikuu vya Georgia na Pennsylania ambao unajumuisha masuala kadhaa ikiwemo maambukizi na matibabu, uwezo wa hospitali na utekelezaji wa njia salama za mazishi. Liberia pia imefanikiwa kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa wa Ebola, hivyo kuongeza uwezo wa hospitali zake kuwahudumia wagonjwa wa Ebola. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, kumekuwa na zaidi ya kesi 21,000 za maambukizi ya Ebola pamoja na zaidi ya vifo 8,300 tangu mlipuko huo utokee Afrika magharibi. Nchini Liberia pekee jumla ya watu 3,496 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Ugonjwa wa Ebola huenda ukatokomezwa Liberia mwishoni mwa Juni mwaka huu

Post a Comment