0

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amekanusha wazo la baadhi ya watu kuwa nchi yake haiko tayari kupambana na makundi yenye silaha ambayo yamesababisha hali mbaya ya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.
Kwenye mazungumzo kati yake na waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini Bw. Novisise Mapisa-Nqakula, rais Kikwete ameeleza msimamo wa Tanzania kuwa itaendelea kujiunga na vikosi kutoka Afrika Kusini na Malawi chini ya Tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa ili kuondoa makundi yenye silaha nchini DRC.

Post a Comment

 
Top