Kwenye hotuba yake kwa taifa, Hollande amewataka raia wa nchi hiyo kuonyesha umoja katika kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Wayahudi siku moja tu baada ya kuuawa kwa kaka wawili waliohusika kwenye mashambulizi ya jana.
Cherif Kouachi na Said Kouachi ambao ni kaka wawili waliohusika na mashambulizi ya Ijumaa katika ofisi za gazeti la Charlie Hebdo, waliuawa jana mchana baada ya kuvamiwa na vikosi vya usalama ndani ya kiwanda cha uchapishaji walimokuwa wamejificha.
Watu 17 wameuawa kwenye mashambulizi hayo yaliyodumu siku tatu nchini Ufaransa.
Post a Comment