Home
»
KITAIFA
» WATU ZAIDI YA 25 WAJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI YA COSTA SENJELE MBEYA.
|
Baadhi ya majeruhi wakitafuta mizigo yao mara baada ya kutoka ndani ya basi hilo
|
|
Baadhi ya majeruhi wakitoka ndani ya basi hilo |
|
Baadhi
ya abilia wakitaka kumpiga Dereva wagari ya aina ya Suzuki kuwa yeye
ndio alisababisha ajali hiyo kwa kuyumbayumba kwake barabarani |
|
Moja
ya wasamaria wema akiwazuia abiria wenye hasira kali kutaka kumpiga
mzee huyo Mwenye Suzuki ambae alijulikana kwa jina moja tu mzee Mtawa |
|
Mwandishi
wa habari Kenneth Mwazembeakiwasili katika Hospitali ya Ifisi
akisindikizwa na Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu baada ya kupata ajali
eneo la Senjele wilayani Mbozi akiwa anatokea shambani kwake huko
wilayani Momba kwa taarifa za awali inasemekana amevunjika mguu wa
kushoto |
|
WATU
zaidi ya 25 wajeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jana baada ya
gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Costa kutoka Mbozi kuelekea
Mbeya kupinduka katika eneo la Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya.
Ajali
hiyo ilihusisha gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 336 CJY
ambalo lilipinduka baada ya kumshinda dereva wakati akijaribu kulikwepa
gari linguine aina ya Suzuki lenye namba za usajili T 327 ARZ.
Kwa
mujibu wa baadhi ya majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo walisema
chanzo ni dereva kushindwa kulimudu gari la abiria baada ya kulikwepa
gari dogo kutokana na kuwa na mwendokasi pamoja na mvua kubwa iliyokuwa
ikiendelea kunyesha.
Baadhi
ya majeruhi walikimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi na wengine
wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu
zaidi.
|
Post a Comment