0
Kipa Juma Kaseja si miongoni mwa wachezaji ambao Yanga itawatumia katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya miamba hao wa soka nchini kuamua kutolipeleka jina lake kwenye Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kaseja ambaye yuko katika mgogoro na klabu hiyo ya Jangwani hayumo katika orodha ya majina ya wachezaji 24 ambao Yanga imewaombea usajili CAF.

Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam ambao wataiwakilisha nchi katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika nao wamepeleka majina 24 CAF.

Mwisho wa kuwasilisha CAF majina ya wachezaji kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho barani mwaka huu ilikuwa juzi Desemba 31 na kuwasilishwa kwa majina 24 ya vikosi vya Azam FC na Yanga kunavifanya klabu hizo kuwa na uwezo wa kuongeza wachezaji sita kila moja kabla ya Januari 15 kukiwa na penalti pia ya CAF kwa timu inayochelewa.

Azam imepangwa kuanza na mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu ya Sudan, El Merrikh katika hatua ya awali ya Klabu Bingwa Afrika wakati Yanga imepangwa kuchuana na BDF XI ya Ligi Kuu ya Botswana katika hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho. Azam na Yanga wote wataanzia nyumbani.

Kikosi cha Yanga kilichowasilishwa CAF kwa mujibu wa taarifa ambazo NIPASHE ilizinasa jana, kina Ally Mustafa 'Barthez', Salum Telela, Rajab Zahir, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima, Sherman Kpah, Jerson Tegete, Juma Abdul, Pato Ngonyani, Nizar Khalfan, Mrisho Ngasa na Alphonce Matogo.

Wengine ni Amissi Tambwe, Hussein Javu, Said Juma, Nadir Haroub 'Cannavaro', Danny Mrwanda, Hassan Dilunga, Simon Msuva, Edward Charles na Deogratius Munishi 'Dida'.

Kikosi cha Azam FC kina Mwadini Ali, Gadiel Michael, Shomari Kapombe, Serge Wawa, Erasto Nyoni, Kelvin Friday, Salum Abubakar 'Sure Boy', Khalid Haji, Kipre Tchetche, Didier Kavumbagu, David Mwantika, Aggrey Morris na Amri Kiemba.

Wengine ni Said Morad, Frank Domayo, John Bocco, Yahya Mudathir, Brian Majwega, Khamis Mcha, Himid Mao, Gaudence Mwaikimba, Waziri Salum, Aishi Manula na Wilfred Michael Bolou.

Post a Comment

 
Top