Huku
zikiwa zimepita saa chache tangu wawashuhudie mahasimu wao kwenye mbio
za ubingwa wa ligi ya Hispania Real Madrid wakipoteza kwenye mchezo wao
wa kwanza wa ligi kwa mwaka 2015 , Fc Barcelona walijikuta wakikutana na
kichapo kama cha wenzao Madrid baada ya kukubali kipigo cha 1-0 mbele
ya Real Sociedad.
Dalili za mwanzo mbaya kwa Barca zilionekana tangu mapema baada ya
beki wa kushoto Jordi Alba kujifunga mwenyewe kwa kichwa akiwa kwenye
harakati za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa toka upande wa kulia .
Bao hili lilidumu hadi mwisho wa mchezo huku Real Sociedad walio
chini ya kocha wa zamani wa Manchester United David Moyes wakikomaa na
kuwazuia Barcelona katika shambulizi walilopanga .
Wachezaji wa Real Sociedad wakishangilia baada ya beki wa Barcelona
kujifunga .Pamoja na ukweli kwamba wengi watashangazwa na matokeo haya ,
ukweli ni kwamba takwimu hazikuwa na ishara nzuri kwa Barcelona kwani
mabingwa hawa wa zamani wa ulaya hawajawahi kushinda mchezo wowote
kwenye uwanja wa Real Sociedad Estadio Annoetta tangu mwaka 2008 ambapo
katika michezo mitano iliyopita walifungwa mara nne huku wakitoka sare
mara moja .
Kipigo hiki kimewanyima Barcelona fursa ya kupanda kileleni mwa
msimamo wa ligi ya Hispania baada ya kuwashuhudia wapinzani wao Madrid
wakipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Valencia.
Kocha wa Sociedad David Moyes akiwa kwenye harakati za kuwaelekeza wachezaji wake kwenye mchezo dhidi ya Barcelona.
Benchi la Barcelona wakati wa mchezo dhidi ya Real Sociedad.Kwa
matokeo haya Real Madrid wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 39
wakiwazidi kwa pointi moja wapinzani wao Barcelona wenye pointi 38 sawa
na mabingwa watetezi Atletico Madrid japo vijana wa Carlo Ancelotti wana
faida ya mchezo mmoja mkononi ambao endapo watashinda wataomgeza
tofauti ya pointi baina yao na wapinzani wake wa karibu kwa pointi tatu
zaidi.
Msimamo wa ligi ya Hispania kama ulivyo baada ya michezo ya wikiendi hii




Post a Comment