Chanzo
cha vurugu hizo kinadaiwa kuwa ni kukatwa mkono kwa mkulima mmoja
aishiye Kijiji cha Mketeni wilayani Kiloasa wakati akibishana na mfugaji
ambaye ni kabila la Kimasai kuhusu eneo la kulishia mifugo.
Kufuatia kitendo hicho cha kukatwa mkono, mkulima huyo aliwafuata
wenzake na kuwapa taarifa ambapo walikusanyika na kuanzisha vurugu dhidi
ya wafugaji wa eneo hilo.Baada ya kuona kuwa bado haitoshi na baadhi ya
wafugaji kukimbia, wakulima walimalizia hasira zao katika Barabara ya
Morogoro - Dodoma ambapo waliamua kuifunga kwa takribani masaa mawili
huku wakichoma matairi
Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliingilia kati na
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima ambao pia walikuwa tayari
wamevamia baadhi ya nyumba za kulala wageni zinazomilikiwa na wafugaji
eneo hilo na kufanya uharibifu.
Majeruhi katika vurugu hizo wamepelekwa hospitali kwa huduma ya kwanza.
Post a Comment