Ujumbe
wa Watalaamu wa masuala wa ICT, Ulinzi na Ujenzi kutoka Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA) uko kwenye ziara ya mafunzo ( Study tour ) katika
Mamlaka ya Bandari Ghana (GPHA) ili kubadilishana utaalamu wa namna ya
kuongeza ufanisi wa utekelezaji na kuimarisha Ulinzi wa Bandari, ujumbe
wa TPA unaongozwa na Ndg. Phares Magesa Mkurugenzi wa ICT - TPA .
Kwa
sasa TPA inatekeleza miradi kadhaa ya kuongeza ufanisi kwa kutumia ICT,
kuboresha Ulinzi kwa kufunga Mitambo ya kielektroniki na kuongeza
vifaa na maeneo ya operations ikiwa ni pamoja na upanuzi wa bandari za
Dar, Mtwara na Ujenzi wa bandari mpya Bagamoyo na Mwambani Tanga.
Ujumbe
wa TPA ukiongozwa na Ndg. Magesa wakiwa kwenye mazungumzo na wenyeji
wao kutoka Mamlaka ya Bandari ya Ghana kufanya majumuisho ya ziara .
Watalaamu wa TPA wakiwa kwenye chumba Chenye vifaa vya kielektroniki
Cha kuangalia matukio ya kuilinzi na ki usalama katika Bandari ya Tema
Watalaamu
wa TPA toka idara za Ujenzi, TEHAMA na Ulinzi wakiangalia Ujenzi wa
Magati manne ya kisasa katika Bandari ya Tema , Ghana
Watalaamu
wa TPA wakiangalia lango la kuingia bandarini ambazo lina vifaa maalumu
vya ki electronic vya kutambua magari, makasha na dereva bila
kusimamia.
Post a Comment