Tanzania
ndiyo nchi pekee ambayo bado inayowauzia wananchi wake mafuta kwa bei
ya juu licha ya kuwa bei ya mafuta katika soko la dunia kushuka kwa
zaidi ya asilimia 50.

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.
Mbunge
wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ameyasema hayo wakati akiongea na
Wananchi wa Halmashauri ya mamlaka ya mji mdogo wa Kyela na kusema kuwa
kumekuwepo na bei kubwa ya mafuta nchini ikilinganishwa na nchi
nyingine.
Mh. Mbilinyi, amedai kuwa bei hiyo ya mafuta ni kubwa ukilinganisha na nchi nyingine duniani ambazo gharama za mafuta imeshuka zaidi ya nusu kutoka na kupatika kwa wingi kwa bidhaa hiyo kwa sasa duniani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la China amesema kuwa katika maeneo ambayo Chadema imeshinda kuongoza serikali za mitaa na vijiji, viongozi wake watafanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya wananchi na sio maelekezo kutoka serikali ku.
Nao viongozi wa Ukawa mkoani Mbeya wamesema kuwa muungano wa vyama vinavyounda umoja huo umeonesha mafanikio makubwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na moto huo huo utaendelea mpaka kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Post a Comment