Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shabaani Mwinjaka
wa pili kutoka (kulia)akipata maelezo kutoka kwa Muongoza ndege kiwanja
cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNIA) Mossy Kitangita wakati
alipotembelea banda la Mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA) . Maonyesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Usafiri wa anga duniani maadhimisho
hayo yanafanyika kwa siku tatu makao makuu ya TCAA jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa bodi wa TCAA, DK. Nyamajeje Weggoro Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Charles Chacha.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye maonyesho ya wiki ya usafiri wa anga Duniani wakipata
maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa TCAA, maadhimisho hayo
yanafanyika kwenye viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa
Angali (TCAA) .jijini Dar es Salaam:” kauli mbiu ikiwa ni “ Miongo saba
ya ushirikiano wa maendeleo ya Usafiri wa Anga na kusherekea miaka
Sabini ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye maonyesho ya wiki ya usafiri wa anga Duniani wakipata maelezo wakati wa maadhimisho
hayo yanafanyika kwenye viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri
wa Angali (TCAA) .jijini Dar es Salaam:” kauli mbiu ikiwa ni “ Miongo
saba ya ushirikiano wa maendeleo ya Usafiri wa Anga na kusherekea miaka
Sabini ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago.
Mkurugenzi
wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Moses Malaki
(kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt.
Shabaani Mwinjaka wa pili kutoka (kushoto ) juu ya huduma wanazotoa maadhimisho
hayo yanafanyika kwenye viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri
wa Angali (TCAA) .jijini Dar es Salaam:” kauli mbiu ikiwa ni “ Miongo
saba ya ushirikiano wa maendeleo ya Usafiri wa Anga na kusherekea miaka
70 ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago. Kutoka Kushoto ni Kaimu mwenyekiti wa bodi wa TCAA, DK. Nyamajeje Weggoro
, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Charles
Chacha,Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Mtesigwa Maugo.
Mhandishi wa ndege wakala
wa ndege za serikali Trophese Mbwambo akimuelezea huduma zinazotolewa
na wakala ndege za serikali Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Dk. .
Shabaani Mwinjaka wakati wa maadhimisho ya wiki ya usafiri wa anga dunuani yanayofanyika kwenye viwanja
vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Angali (TCAA) .jijini Dar es
Salaam:” kauli mbiu ikiwa ni “ Miongo saba ya ushirikiano wa maendeleo
ya Usafiri wa Anga na kusherekea miaka 70 ya Mkataba wa Kimataifa wa
Chikago.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Dk. . Shabaani Mwinjaka (katikati) na Kaimu mwenyekiti wa bodi wa TCAA, DK. Nyamajeje Weggoro wakisisitiza
jambo kwa Kaimu Meneja Huduma za hali ya hewa ya Usafiri wa Anga (TMA)
John Mayunga wakati walipotembelea banda lake kwenye maadhimisho ya wiki
ya Usafiri wa Anga Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Makao makuu
ya Mamlaka ya Usafiri wa Angali (TCAA) .jijini Dar es Salaam:” kauli
mbiu ikiwa ni “ Miongo saba ya ushirikiano wa maendeleo ya Usafiri wa
Anga na kusherekea miaka 70 ya Mkataba wa Kimataifa wa Chikago.
Tanzania
inaungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya
usafiri wa anga, (International Civil Aviation Day) ambayo huadhimishwa
Desemba 7 kila mwaka. Lengo la maadhimisho hayo ni kukuza uewelewa wa
wananchi kuhusu sekta ya usafiri wa anga na namna inavyochangia
maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mataifa mbalimbali.
Mwaka huu
siku hiyo inaadhimishwa ikiwa ni miaka sabini (70) tangu kupitishwa na
kusainiwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa Usafiri wa Anga (maarufu
kama Chicago Convention) na tangu kuanzishwa kwa Shirika la Kimataifa la
Usafiri wa Anga (ICAO).
Kauli
mbiu ya maadhimisho kwa mwaka huu ni “Miongo Saba ya Ushirikiano wa
Maendeleo ya Usafiri wa Anga na Kusherehekea Miaka Sabini ya Mkataba wa
Kimataifa wa Chikago”.
Kwa
Kiingreza: “Celebrating Seven Decades of Cooperative of Air Transport
Progress and Celebrating 70 years of Chicago Convections.”
Mamlaka
ya Usafiri wa Anga (TCAA) kwa kushirikiana na wadau wa sekta wameandaa
shughuli mbali mbali kuadhimisha miaka sabini ya usafiri wa anga
duniani. Kwa vile tarehe 7 Desemba ni siku ya Jumapili, maadhimisho
yetu yatafanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Desemba.
Moja ya
Shughuli zitakazofanyika katika kipindi cha maadhimisho ni maonyesho ya
wadau wa usafiri wa anga kwa siku tatu, kuanzia tarehe 3 hadi 5 Desemba
katika viwanja vya Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Banana-
Ukonga.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba, anatarajiwa kuwa mgeni ramsi
katika maonyesho hayo yanayolenga kutangaza shughuli za wadau wa sekta
ya usafiri wa anga. Wadau hao ni pamoja na vyuo vya usafiri wa anga,
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, makampuni ya ndege, Mdhibiti wa sekta na
wadau wengine wanaotoa huduma kwenye viwanja vya ndege wakiwemo
Swissport na Equity Aviation.
Tarehe 4
Desemba kutakuwa na kongamano la wadau wa sekta, litakaloongozwa na
kauli mbiu “Miaka 70 ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga-
Mikakati ya Tanzania Katika Kuimarisha Maendeleo ya Usafiri wa
Anga”. Pamoja na mambo mengine kongamano litaangalia mbinu za kuimarisha
sekta ya usafiri wa anga nchini, mchango wake katika kukuza uchumi,
kinga ya abiria dhidi ya majanga, mchango ya huduma ya hali ya hewa
kwenye usafiri wa anga pamoja na changamoto zinazokabili sekta hii.
Kongamano litafanyikia ukumbi wa mikutano, Makao Makuu ya Mamlaka ya
Usafiri wa Anga na kufunguliwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dr. JUma Malik Akil.
Katika
maadhimisho haya, pia kutakuwa na safari maalum ya ndege kutoka Dar es
Salaam kwenda Zanzibar kwa kundi la watoto 20 wakiwemo wanafunzi
waliofanya vizuri kimasomo na wale wa kundi la mazingira maalum. Safari
imelenga kuchochea udadisi wa watoto kwenye sekta ya usafiri wa anga na
kuwaamasisha ili wasome zaidi na hatimae kuja kutumikia sekta ya usafiri
wa anga.
Waziri wa
Uchukuzi, Mh. Dr. Harrison Mwakyembe, ambaye atakuwa Mgeni Rasmi siku
ya kilele cha maadhimisho, tarehe 5 Desemba, atatembelea na kukagua
maendeleo ya baadhi ya miradi katika sekta ya usafiri wa anga. Miradi
atakayoikagua ni pamoja na Mradi wa Swissport unaohusisha ujenzi wa
Bohari Maalumu la mizigo inayosafirishwa na usafiri wa anga ambayo ina
uwezo wa kutunza wanyama hai. Tanzania kwa mara ya kwanza itakua na
huduma za kuhifadhi wanyama hai wanaosubiri kusafirishwa au kupokelewa
kupitia usafiri wa anga. Mh Waziri pia atapata nafasi ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Jumba la Abiria (Terminal 3) katika Kiwanja cha
Ndege cha Julius Nyerere. Aidha, Mh. Waziri atazindua Makao Makuu ya
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania- TCAA, yaani Aviation House.
Kamati ya
wadau ya maandalizi inawakaribisha wananchi wote kuhudhuria kwenye
maonyesho na kutumia fursa hiyo kujifunza zaidi kuhusu sekta ya usafiri
wa anga na mchango wake katika maendeleo ya huduma na uchumi wa nchi
yetu. Makampuni ya ndege yanatarajiwa pia kuchukua nafasi hiyo kutoa
huduma zao za tiketi wakati wa maonyesho.
Post a Comment