
Amri imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwa ferry iliyo na
karibu abiria 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini
Ugiriki kwenda Italia.
Abiria waliokuwa kweye ferry hiyo walipiga simu kwa vituo vya runinga
nchini Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na upepo unatatiza shughuli
za uokoaji.
Maafisa wa ulinzi wa pwani nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya
Norman Atlantic ilikuwa umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi
wakati walipotuma ujumbe.
Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari.
Post a Comment