Polisi mjini Mombasa Pwani ya Kenya
wanasema wamepata silaha nyingine zaidi ikiwemo mabomu katika msikiti wa
tatu ambao ulifanyiwa msako Mtaa wa Kisauni ndiko vijana waliokuwa wamejihamu kuwadunga visu watu wanne na kuwaua. Pia waliwashambulia kwa silaha nyingine gutu.
Waziri wa usalama wa ndani, Joseph Ole Lenku anasema kuwa msako huo ulifanywa katika misikiti ambayo hutumiwa na watu wanaoeneza itikadi kali za kiisilamu kwa vijana ambao inadaiwa wanajiunga na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab nchini Somalia.
Viongozi wa kiisilamu wamelanaani misako hiyo katika msikiti wakisema kuwa itachochea zaidi vijana kuendeleza itikadi kali za kidini.
Post a Comment