Waumini wa kiisilamu wakifanya maandamano kupinga unyanyasaji Mombasa.Polisi nchini Kenya wanasema kuwa wamenasa maguruneti na silaha nyinginezo usiku wa kuamkia leo katika msako mkali walioanza kufanya dhidi ya misikiti inayodaiwa kutoa mafunzo ya itikadi kali za kidini mjini Mombasa pwani ya Kenya.
Mtu mmoja aliuawa na wengine zaidi ya 250 kukamatwa katika msako huo unaolenga misikiti inayosemekana kutoa mafunzo kusiana na harakati za wapiganaji wa kiisilamu wa Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi wanadai kuwa misikiti hiyo ikiwemo Masjid Musa inatumika kwa kuwasajili vijana wanaojiunga na Al Shabaab nchini Somalia.
Msikiti mwingine uliolengwa ni ule wa Sakina.
Mkuu wa polisi mjini Mombasa alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa walipata taarifa kwamba kundi hilo limekuwa likipanga kufanya mashambulizi na hiyo ndio sababu ya msako huo kuanzishwa.
Viongozi kadhaa wa kiisilamu wameuawa mjini Mombasa hivi karibuni
Post a Comment