Polisi wa
kutuliza ghasia, wakifanya doria kwenye mitaa ya jiji la Mwanza baada
ya kutokea ghasia kufuatia askari wa jiji hilo kufanya jaribio la
kuwaondoa wamachinga kwenye soko kuu, rwagasore na mtaa wa Lumumba
mapema Jumatano Novemba 19, 2014
Polisi wa
kutuliza ghasia wakiwa wamejihami kwa silaha wakati wakituliza ghasia
za wamachinga kwenye mitaa ya jiji hilo mapema leo Jumatano Novemba 19,
2014. Zogo hilo lilizuka baada ya askari wa jiji walipowavamia
wamachinga na kuwaamuru waondoke kwenye maeneo ya soko kuu, Rwagasore na
mtaa wa Lumumba na hapo ndipo "Kasheshe" lilipozuka ambapo askari wa
jiji walizidiwa nguvu kutokana na mawe yaliyokuwa yakirushwa na
wamachinga mithili ya maroketi na kuwafanya warudi nhyuma na ndipo
polisi wa kutuliza ghasia walipoitwa na kuwakabili wamachinga hao.
Moja ya
barabara za jiji la Mwanza ikionekana kuwa nyeupe huku watu wachache
wakitafuta mahala salama baada ya polisi kupambana na wamachinga mapema
leo Jumatano Novemba 19, 2014
Machinga,
akirusha jiwe, wakati polisi wa kutuliza ghasia walipoingia mtaani na
kupambana na wafanyabiashara ndogondogo jijini Mwanza maarufu kama
wamachinga, leo Jumatano Novemba 19, 2014
Post a Comment